KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA CHUNYA,KESHO NI MBARALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA CHUNYA,KESHO NI MBARALI

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisogeza matofali kwa Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kuyapandisha juu kwa ajili ya ujenzi wa soko la Mulugo Market Mwambani lililopo katika ya kata Mwambani wakati viongozi hao waliposhiriki ujenzi wa soko hilo linalojengwa na Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mh. Philip Mulugo katika kuwakwamua kiuchumi wananchi wa jimbo la Songwe wilayani Chunya, Kinana amemaliza ziara yake katika wilaya hiyo na kesho anaanza ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya. 2Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Maweni kata ya Mwambani wilayani Chunya kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo lililojengwa kwa msaada wa Shirika la maendeleo la watu wa Japan (JAICA) kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi. 3Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutokam kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Maweni wakati alipokagua ujenzi wa bweni la wanafunzi
katika shule hiyo.  6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi ya Saza katika kata ya Saza Mkwajuni Chunya, anayeshuhudia ni mkuu wa
mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro.
8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wafugaji katika kijiji cha Mteka kata ya Kapalala. 9Wafugaji wa kijiji cha Mteka kata ya Kapalala wilayani Chunya wakimpokea kwa ushujaa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana huku wakiimba nyimbo za kumsifu wakati alipowasili katika kijiji hicho cha wafugaji. 10Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa ajili ya kulnywesha mifugo yao lakini pia kutumia kwa shughuli za kibinadamu kisima hicho kimefungwa mitambo inayovutamaji kwa kutumia upepo Power Wind, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Mh. Godfrey Zambi. 11Kisima chenyewe ndiyo hiki. 12wafugaji wakifurahia jambo wakati Kinana alipokuwa akiongea nao. 13Abdulrahman Kinana akiuliza jambo wakati akikagua maradi huo katika eneo la matanki ya maji. 15Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende mara baada ya kuzindua mradi
huo.
16 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiongoza na wafugaji kuelekea eneo la kunweshea mifugo.
17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiuliza jambo kutoka kwa injinia wa idara ya maji Wilaya ya Chunya Bw
Ndele Mengo wakati akikagua lambo hilo la kunyweshea
mifugo.
18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,
katikati Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo kulia na Nape
Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakila chakula
kilichoandaliwa na jamii hiyo ya wafugaji kwa ajili ya wageni.
19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya
Kapalala kata ya Kapalala ambalo linajengwa na wakulima wa Tumbaku
kupitia taaisis yao ya Chunya Development Trust.
20Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo
kushoto na mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro kulia
wakishiriki kazi ya kusomba tofali katika ujenzi wa bweni la shule ya
sekondari ya Kapalala wilayani Chunya,
22Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo
akizungumza na wananchi wa Udinde mahali ambapo ndipo alipozaliwa
wakati wa mkutano wa hadhara leo.
23Wananchi walipanda hata kwenye miti ili
kumshuhudia katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji
cha Udinde.
25Katibu wa CCM wilaya ya Chunya Braison
Mwasimba aliyejejea CCM jana akiwapa ukweli wananchi wa kijiji cha
Udinde.
26
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubiwa wananchi wa kijiji cha Udinde Mkwajuni leo.
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MKWAJUNI-CHUNYA) 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages