Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani Bw. Akpor Otebele, akiongea kwenye semina hiyo jijini Arusha leo
Juu na chini ni washiriki wa semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, iliyoandaliwa na Tamasha la Filamu za Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013)
WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga neno la ‘WOOD’, kwenye soko la filamu hasa baada ya nchi nyingi kukopi jina la ‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu.
Akielezea mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele, alisema Waafrika waache dhana ya kuendelea kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia viunganishi vya neon hilo la ‘Wood’ bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia.
Hii haina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji wengi wanatafakari maana ya hili neno lakini jibu hakuna, lakini bado wanaendelea kulitumia” alisema.
Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tanzania), Nollywood (Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sierra Leone)na Congowood (Kongo) na mengine mengi.

Akpor Otebele aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani, ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya.
…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is that sure? So why to use ‘Wood’?? in Swahili meaning ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.
…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is that sure? So why to use ‘Wood’?? in Swahili meaning ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)