KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AICHANA CHADEMA TUNDUMA-MOMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AICHANA CHADEMA TUNDUMA-MOMBA

1Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana jioni ya leo, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma, ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi. Katika mkutano huo uliofabnyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, Kinana aliambatana na majenbe ya Chama cha Mapinduzi , Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Katika mkutano huo Kinana amesema wananchi kuikosoa CCM sio kosa kwani Chama hicho kimeingia mkataba na wananchi pale kilipopewa ridhaa ya kuongoza nchi ili kutekeleza ilani yake ya uchaguzi na ni haki ya mtu yeyote wakiwemo wapinzani ili kujua maendeleo yao, Amesema CCM haitakubali kuona ukiritimba na umangimeza wa baadhi ya watendaji Serikalini na unakwamisha maendeleo ya wananchi, ameongeza kuwa kazi ya CCM ni kutenda tu na kazi ya wapinzani ni kusema maneno tu.
2Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini
Tunduma.
3Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 4Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amebebwa juujuu na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo. 5Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisakata muziki na wakina mama wana CCM kabla ya kuanza kwa mkutano huo. 6Wananchi wakisakata muziki kabla ya kuanza kwa mkutano.

7Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiskata muziki na wananchi 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akilekea katika eneo la mkutano
10aMsafara ukiwasili mjini Tunduma ukitokea wilayani Ileje 11Maelefu ya wananchi wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana hayupo pichani alipokuwa akiwahutubia.12Hapa akisisitiza jambo kwa wananchi hao wakati akitoa hutuba yake
13
Mzee wa kimila wa kabila la wanamwanga wilayani Momba Jubeki Chipansia akimpa silaha za kijadi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumsimika kuwa miongoni mwa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduma leo jioni. PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-TUNDUMA-MOMBA 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages