ASIA IDOROUS KUPAMBA UZINDUZI WA ‘KIOTA’ KIPYA CHA CLUB TIFFANY - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ASIA IDOROUS KUPAMBA UZINDUZI WA ‘KIOTA’ KIPYA CHA CLUB TIFFANY

Na Mwandishi Wetu
WADAU mbali mbali wa burudani  na mitindo nchini ususani wa jijini Dar es Salaam,  wanatarajia kushuhudia shoo kali ya onesho la mavazi kwenye uzinduzi wa  ‘kiota’ kipya cha burudani cha Club Tiffany.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Usiku wa Ijumaa Novemba 29,  ndani ya  hoteli ya  kisasa ya Tiffany Diamond , iliyopo katikati ya jiji la Dar e Salaam Mitaa ya Morogoro na Indira Gandi huku kiingilio kiasi cha sh. 10,000.

Akizungumzia  kupamba shoo hiyo, Asia Idorous, alisema tayari warembo wake wamejifua vya kutosha kuonesha mavazi mavazi mapya nay a kisasa ndani ya Club hiyo.

“Mamodols wamejipanga kuonesha shoo ya pekee na ya aina yake kwenye uzinduzi huo, hivyo wadau wa burudani na mitindo watafurahia shoo hiyo naomba wajitokeze kwa wingi” Alisema Asia Idorous. Na kuongeza kuwa,  mbali na shoo hiyo, pia kutakuwa na utambulisho wa Tanzania Top Model, watakaoongozwa na mshindi wa Mr. Dar 2013.

Ukumbi huo wa kisasa upo ndani ya hoteli hiyo ya Tiffany Diamond,  kwenye ghorofa ya 10, ambapo umejengwa kwa mtindo wa kisasa na kuwa ukumbi wa kipee kwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages