ANGEL AWAOMBA WATANZANIA KUMNUSURU KIKAANGONI, TUSKER PROJECT FAME - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ANGEL AWAOMBA WATANZANIA KUMNUSURU KIKAANGONI, TUSKER PROJECT FAME

 Angel and Fess walk into Club Samba to perform and meet fans

Ili kumpigia kura tuma neno ‘Tusker 14’ kwenda namba 15324
Mshiriki kutoka Tanzania Angel Karashani (Angel) anawaomba watanzania kumpigia kura kwa wingi ili aendelee kubaki katika mashindano hayo ya Tusker Project Fame 6. Angel ameonesha jitihada zake katika kujikomboa na hatari ya kutolewa katika shindano hilo siku ya jumamosi ambapo washiriki walioko kikaangoni katika mashindano ya Tusker Project Fame nchini Kenya watarudia nyimbo zao ili kurekebisha walipokosea wiki iliyopita na watakaoshindwa kumudu zoezi hilo watayaaga rasmi mashindano.

Angel ameonesha kujifua kiasi cha kutosha huku akiwataka watanzania tumpe ushirikianao kwa kumpigia kura ili aendelee kubaki katika shindano hilo. Ili tumuokoe katika kutolewa watanzania tunaombwa kuonyesha ushirikianpo kwa kumpigia kura mara nyingi tuwezavyo kwani bila shaka ataendelea kuipeperusa bendera ya nchi yetu. Ili kumpigia kura unaombwa kutuma neno ‘Tusker 14’ kwenda namba 15324.

Katika mazoezi yanayoendelea kwa washiriki walioko katika hatari, Angel ameonekana akijitahidi kufuata maelekezo ya mwalimu wake. Angel alipata fursa ya kuonesha kile alichokiweka katika uimbaji wake kwa mwalimu Erick hivyo kujipatia nafasi ya kukoselewa zaidi na kupewa moyo, juu ya sauti yake kuwa ni nzuri na anastahili kubaki katika mashindano hayo iwapo ataongeza bidii.

Nae meneja wa bia ya Tusker inayotengenezwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Sialouise Shayo amempongeza mshiriki Hisia ambae anaiwakilisha vyema Tanzania huku akiwasisitiza watanzania kumpigia kura mshiriki Angel ili aweze kubaki katika mashindano hayo na kuendelea kupeperusha bendera ya nchi yetu kwa kuwa kipaji anacho na anaimba vizuri kikubwa ni kumpa moyo. “Sisi kama wadhamini wa shindano hili tunajivunia sana uwepo wa watanzania Hisia na Angel katika mashindano haya ya Tusker Project Fame msimu wa sita kwani ni faraja kubwa kwetu na kwa watanzania wote. Kikubwa ni kumpa ushirikiano Angel kwa kumpigia kura nyingi zaidi”. Alieleza meneja huyo.

Washiriki walioko kikaangoni walijipatia fursa ya kupelekwa katika matembezi na kufanya manunuzi mbalimbali, washiriki Angel kutoka Tanzania, Phionah kutoka Rwanda pamoja na Fess kutoka Kenya walionesha kufurahia zaidi matembezi hayo huku wakinunua vitu mbalimbali. Jennifer pia kutoka Kenya alionesha kufurahia zaidi japokuwa yupo kikaangoni kwa mara ya pili katika mashindano hayo.

Usikose kutizama mashindano haya moja kwa moja kupitia televisheni ya East Afrika TV kuanzia saa 2:00 usiku siku ya Juma mosi pamoja na Jumapili saa 1:30 usiku pia kuanzia saa 4:00 usiku kupitia televisheni ya ITV.


 Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako, tafadhali kunywa kistaarabu haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.//

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages