ALEX MSAMA AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA TAMASHA LA KRISMAS DESEMBA 25 /2013 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ALEX MSAMA AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA TAMASHA LA KRISMAS DESEMBA 25 /2013

1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama amezungumza na waandishi wa habari leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam na kuelezea maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika siku ya sikukuu ya Krismas kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa injili kutoka ndani na nje ya Tanzania ametaja nchi ambazo washiriki watatoka kuwa ni Tanzania yenyewe, Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Ameongeza kuwa mmoja wa waimbaji hao kutoka Zambia natatarajia kuzindua albam yake mpya katika tamasha hilo. Msama pia amesema nusu ya fedha zitakazopatikana zinatarajia kulipia karo za shule kwa watoto wasiojiweza wapatao 300 na fedha nyingine zitaelekezwa kwenye ujenzi wa kituo cha misaada kwa w asiojiweza kitakachoitwa Jakaya Mrisho Kikwete Rafiki wa wasiojiweza kinachotarajiwa kujengwa huko Pugu, Kauli Mbiu ya Tamasha hilo ni "TANZANIA NI YA WATANZANIA TUILINDE NA KUIDUMISHA AMANI YETU" 2Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari wakati akizungumzia maandalizi ya Tamasha la Krismas kwenye viwanja vya Karimjee leo. 3Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -KARIMJEE 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages