Pages

Van Persie, Thabeet wala bata Manchester

 
Hasheem Thabeet akipozi na mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie.
 
Na Mwandishi Wetu
MTANZANIA anayecheza kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabeet, alijumuika pamoja na mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie na kula ‘bata’ pamoja.
Akizungumza juzi usiku kutoka jijini Manchester, England, Thabeet alisema walikutana usiku katika klabu na kustarehe pamoja kwa saa kadhaa.

“Ilikuwa ni siku nzuri, tulijumuika pamoja. Nilikuwa na wachezaji wenzangu wa OCT (Oklahoma City Thunder). Yeye pia alikuwa na wenzake wa Manchester. “Tukajumuika pamoja, zikawa meza tofauti ila mimi nikawa na van Persie,” alisema Thabeet ambaye ndiye mwanamichezo nyota zaidi wa Tanzania katika kipindi hiki.

Thabeet aliyechipukia kwenye mchezo wa kikapu katika timu ya UDSM, alikuwa jijini Manchester kwa ajili ya tamasha la NBA Global Games na walicheza na timu nyingine ya Marekani ya Philadelphia 76ers.

Pamoja na tamasha hilo, kikosi cha Thunders anachochezea Thabeet kilikuwa katika maandalizi ya kabla ya msimu wa NBA unaotarajiwa kuanza ndani ya wiki chache zijazo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)