Pages

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA KWA UMMA-AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI

DSC00260 MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA RELINI – MLOWO  BARABARA YA  MLOWO/KAMSAMBA  WILAYA YA  MBOZIMKOA WA MBEYA. GARI T.353 APR AINA YA  TOYOTA HILUX P/UP  LIKIENDESHWA NA DEREVA  ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA  MTOTO PETRO S/O KAUNDA, MIAKA 3,  KYUSA, PIA MAJERUHI KWA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AITWAE FAUSTA D/O MBUBA, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITEMPULA AMBAYE AMELAZWA ZAHANATI YA NAZARETH – MLOWO. CHANZO KINACHUNGUZWA.

DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA  KATIKA ZAHANATI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA  MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA  USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA  RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE  KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,  VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA  KYELA  – KUPATIKANA NA BHANGI. MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA MBUGANI WILAYA YA  KYELA  MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRANK S/O ARON, MIAKA 27,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBUGANI   AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 20 SAWA NA UZITO WA GRAM 120. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE  MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA  ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)