TTB YAZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO KUTANGAZA UTALII NJE YA NCHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TTB YAZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO KUTANGAZA UTALII NJE YA NCHI

Mahmoud Ahmad Arusha
Bodi ya utalii Tanzania(TTB)imezindua mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini huku ikieleza mkakati wa kutafuta soko jipya la watalii nchi za China,Japani na Brazil.
 
Meneja utafiti na maendeleo wa TTB Deogratus Malingo akieleza mkakati huo wa TTB katika mkutano na kampuni zinazotoa huduma ka watalii mkoani Arusha alisema TTB imejipanga kuboresha mfumo wa kutangaza Tanzania kam,a moja ya vituo bora vya utalii duniani.
 
Malongo alisema ingawa idadi ya watalii wanaokuja nchini imekuwa ikiongezeka kwa kila mwaka na kufikia 1.2 bado kuna haja ya kuendelea kutangaza vivutio bora vya utalii katika nchi ambazo zinaleta watalii na nyingine ambazo bado watalii wanaofika ni wachache.
 
“Kwa sasa waingereza ndiyo wanaongoza kwa kutembelea Tanzania mwaka jana walikuwa 69,680wakifuatiwa na wamarekani65,110na Waitaliano 50,187 lakini kuna haja ya kujitangaza zaidi nchi hizi na nyingine duniani”alisema Malongo.
 
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa chama cha watoa huduma za utalii Tanzania(TATO)Willy Chambulo alisema sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi.
 
Chambulo alisema kuna urasimu wa kupata vibali gharama kubwa za watalii wanaokuja nchini na kukosekana ndege ya moja kwa moja kutoka mataifa makubwa kama china na kwengineko duniani na kuna haja kwa serekali kuliangalia hilo.
 
“tunaamini serekali ikifanyiakazi tutaweza kuongeza idadi ya watalii na kuongeza pato la taifa na kuna haja ya kuweka mazingira mazuri ya kuweza kupata usafiri wa uhakika kutoka mataifa hayo ilikuweza kupata watalii wengi zaidi”alisema Chambulo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages