KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O MWAMBENJE, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.
MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA, NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA 33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA LUPA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
DIWANI ATHUMANI - ACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)