AMREF TANZANIA, MONTAGE LIMITED NA BENKI M WAANDAA CHAKULA CHA HISANI KWAAJILI YA KUSOMESHA WAKUNGA UTAKAOFANYIKA IJUMAA YA WIKI KATIKA HOTEL YA SERENA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AMREF TANZANIA, MONTAGE LIMITED NA BENKI M WAANDAA CHAKULA CHA HISANI KWAAJILI YA KUSOMESHA WAKUNGA UTAKAOFANYIKA IJUMAA YA WIKI KATIKA HOTEL YA SERENA


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi Teddy Mapunda akieleza jambo mbele ya wahandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tukio muhimu la Usiku wa Chakula Cha Hisani liitwalo Stand Up For Tanzania Mothers litakalofanyika ijumaa ya tarehe 11 Octoba 2013 katika hoteli ya serena Kwaajili ya Kuchangisha fedha ya kuwasomesha Wakunga ili kuweza kutoa Huduma ya mama na mtoto, usiku huo umeandaliwa na Kampuni ya Montage kwa kushirikiana na AMREF, BENKI M huku ikidhaminiwa na ITV, NBC, Serena, Serengeti Brewries, Clouds Fm, Coca Cola, Mbc, Tigo, CBA, Toyota, EXTREME SOLUTION, TACAIDS, MSD, THE GUARDIAN, DSTV, BOT NA SONGAS
 Mwenyekiti wa Benki M upande wa Biashara Bi Jacqueline L Wolso akielezea sababu kwanini Benki M imeamua kushirikiana na Kampuni ya Montage Limited katika kuchangisha fedha kwaajili ya Kusomesha Wakunga ili kuweza kusaidia kutoa huduma ya Mama na Mtoto, usiku wa chakula cha hisani utafanyika katika Hoteli ya Serena tarehe 11 octoba 2013
Mkurugenzi Mkuu wa AMREF Tanzania Dr Festus Ilako akielezea sababu ya AMREF Tanzania kushirikiana na Kampuni ya Montage Limited na Benki M katika Kuanda Usiku wa Chakula Cha Hisani Kwaajili ya Kuchangisha fedha ya kusomesha wakunga ili kuweza kutoa huduma ya Mama na Mtoto Nchini, Usiku wa Chakula Cha Hisani utafanyika katika hotel ya Serena Siku ya Ijumaa tarehe 11 octoba 2013
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage limited Bi Teddy Mapunda akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya mkutano na waandishi wa Habari, mkutano uliofanyika leo katika Hotel ya Serena.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages