Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited(MCL)Tido
Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza
uchapishaji leo wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki
mbili.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis
Msacky(Kulia kwake) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bernard
Mukasa(kushoto)
Mkurugenzi wa Mwananchi, Tido Mhando akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhusiana na kuanza kwa uchapishwaji wa gazeti hilo linalosadikiwa kuuzwa zaidi Tanzania
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu. Kwanza ni gazeti lake mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo, wamechukua fursa na kuongelea kuhusu KUREJEA
KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega kwa bega.
KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega kwa bega.
KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali, kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na uhariri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayou yataendelea kusambazwa nchi nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea kote Tanzania.
Kwa
wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho
watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi
watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao
moja kwa moja.
PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea.
Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)