Benki ya Posta Yatoa Mafunzo kwa Wajasiliamali Dar es Salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Benki ya Posta Yatoa Mafunzo kwa Wajasiliamali Dar es Salaam

IMG_0262
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akizungumza katika semina ya wajasiliamali wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).
IMG_0370
Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akijaza fomu kufungua akaunti ya Huduma Popote inayotolewa na TPB mara baada ya kufungua semina hiyo na kutembelea Tawi la Benki ya Posta Tanzania lililopo Jengo la Ubungo Plaza.
IMG_0332
Mmoja wa maofisa kutoka kitengo cha masoko wa Benki ya TPB, tawi la Kariakoo (kulia) akitoa ufafanuzi kwa mteja kuhusu huduma mpya ya Popote ndani ya semina ya wajasiliamali Ubungo Plaza.
IMG_0391
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Prof. L. Rutashobya (katikati) akikabidhi zawadi ya saa ya ukutani kwa mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) mara baada ya kufungua semina hiyo na kutembelea moja ya tawi la Benki ya Posta Tanzania lililopo Jengo la Ubungo Plaza. Kushoto ni meneja wa tawi la TPB Ubungo Plaza.
IMG_0270
Baadhi ya mameneja na maofisa wa matawi ya Benki ya Posta Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika semina hiyo.
IMG_0220
Baadhi ya wajasiliamali washiriki wa semina ya Benki ya Posta Tanzania (TPB), inayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam leo.
Na Joachim Mushi, Dar

BENKI ya Posta Tanzania (TPB) leo imetoa semina kwa wajasiliamali wake wadogo wadogo wa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wa namna ya uendeshaji biashara zao kwa faida zaidi. Semina hiyo iliyowashirikisha wajasiliamali kutoka maeneo anuai ya jiji la Dar es Salaam imeshirikisha takribani wajasiriamali 150.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika semina hiyo, alisema wajasiliamali watajifunza namna ya kupangilia Mpango wa Biashara, Mbinu za kukuza biashara, Ukopaji bora na Utunzaji wa kubukumbu mambo ambayo ni muhimu kwa kila mjasiliamali.

"Tumegundua umuhimu wa kutoa mafunzo elekezi kwa wateja wetu na hususani wale wanaokopa na leo ndio siku ya uzinduzi wa Mafunzo. Hapa yatatolewa mafunzo kuhusu, Mpango wa Biashara, Mbinu za kukuza biashara, Ukopaji bora na Utunzaji wa kubukumbu tutaendelea na mafunzo hayo katika mikoa yote ya Tanzania, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wateja wetu," alisema Moshingi.

Hata hivyo alisema benki ya Posta itaendelea na utoaji wa mafunzo hayo katika mikoa yote ya Tanzania, huku lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wateja pamoja na wajasiliamali. Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu aliipongeza benki ya Posta kwa kitendo cha kuendelea kuwajali wajasiliamali kwa kuwapa mafunzo kama hayo.

Aidha Teu alisema serikali itaendelea kuziunga mkono juhudi zozote za kuwainua wajasiliamali zinazofanywa na benki kama TPB pamoja na taasisi za fedha ili kumuinua Mtanzania katika kujipatia kipato chake.

Hata hivyo kiongozi huyo aliupongeza uongozi wa TPB kwa kile kuweza kumudu ushindani wa kibiashara, kwani kwa sasa kuna ushindani mkubwa wa mabenki na taasisi za fedha lakini benki hiyo inaendelea kumudu ushindani huo bila kutetereka.

TPB kwa sasa ina jumla ya matawi 29 huku ikiwa na matawi madogo madogo 16 na pia wateja wa benki hiyo wanauwezo wa kupatiwa huduma kwenye ofisi zaidi ya 120 za TPC.

TPB pia ina ATM 25 na ni member wa Umoja Switch yenye ATM zaidi ya 160, huku ikiwa na rasilimali za benki zenye thamani ya sh. bilioni 190 za wateja bilioni 151.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages