Waziri Nchimbi atembelea makao makuu ya NIDA jijini Dar es salaam leo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Waziri Nchimbi atembelea makao makuu ya NIDA jijini Dar es salaam leo


Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Ndugu Dickson Maimu, akimkaribisha Mhe Waziri
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akieleza jambo menejimenti ya NIDA, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, kushoto ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kufanya kikao na Menejimenti ya NIDA Septemba 18,2013.

Dk. Nchimbi katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi.

Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Ujenzi wa Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu na zoezi la Usajili wa watu linaloendeshwa na NIDA ikishirikiana na Serikali za Mitaa, Uhamiaji, RITA na Vyombo vya Usalama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages