Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho
akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha
idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati
mbalimbali ya kimaendeleo.Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
………
Na Magreth Kinabo- Maelezo
KAMISHNA
wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho ametoa
onyo kwa watu wanaotumia takwimu ambazo si sahihi wanapotoa taarifa
mbalimbali kuwa wawe makini kwa kuwa sheria ya kuwabana iko mbioni.
Aidha
Hajjat Amina amesema kwamba kwa watendaji wa Serikali, na wanasiasa
watakaotoa takwimu za uongo katika taarifa mbalimbali wajiandae
kuong’ooka katika nyadhifa zao.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Kamshina huyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha idadi ya watu cha umri na jinsi,
ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
“Muswada
wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 imeshasomwa mara ya kwanza Bungeni
,unasubiriwa kusomwa kwa mara ya pili katika Bunge lijalo. Hivyo
itakapokamilika sisi tutapambana na watu wanaotoa takwimu ambazo si
sahihi. Kwa watendaji wa Serikali watakaotumia takwimu ambazo si sahihi
wakati wanapotoa taarifa mbalimbali mfano tatizo la njaa linawakabili
watu kiwango kipi wajiandae kufukuzwa kazi,” alisema Hajjat Amina.
Alisema
suala linatakiwa pia kuzingatiwa watu wataotangaza au kuandika,wakiwemo
waandishi wa habari takwimu zilizotajwa na mtu bila ya kufanyiwa
uchunguzi kupitia mtandao wa ofisi hiyo watachukuliwa hatua kulingana na
sheria hiyo.
Hajjat
Amina alifafanua kuwa takwimu hizo zitakuwa zitaboreshwa kwa kila
mwaka, hivyo aliwataka watu kuzitumia ipasavyo kulingana na taarifa za
kila mwaka.
Akizungunzia
kuhusu uzinduzi huo, alisema utafanyika Septemba 25, mwaka huu katika
ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dares Salaam,
ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Sief Ali Iddi .
Aidha
Hajjat Amina aliongeza kuwa ofisi hiyo itato vitabu 2 , kitabu cha
tatu kuhusu takwimu za walemavu kifuata kitazinduliwa mwishoni mwa mwezi
wa Okctoba na cha nne kitakachoonesha takwimu za kila mkoa, utakuwa na
chake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)