Mshambuliaji wa Simba SC aliyefunga mabao manne leo, Amis Tambwe.
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Tabwe.
Shabiki wa Simba aliyekuwa Yanga (kushoto mwenye kitambaa kichwani) akishangilia ushindi.
SIMBA SC leo imefanya kweli baada ya kuiporomoshea mvua ya mabao Mgambo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar leo.
Mabao ya Wekundu hao wa Msimbazi yamewekwa kimiani na Amis Tambwe aliyetupia mabao manne, Haruna Chanongo akafunga moja na beki wa Mgambo akawapatia bao la sita kwa kujifunga.
Wakati Simba ikifanya kweli Taifa, watani wake Yanga SC wao wameendelea kupunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare nyingine ya 1-1 na Prisons ya jijini Mbeya. Jumamosi iliyopita Yanga alitoka sare na Mbeya City ya mkoani humo. Huko mkoani Kagera, Kagera Sugar ameibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya JKT Oljoro kwenye mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Kaitaba. Azam FC imekwenda sare ya 1-1 dhidi ya Ashanti mechi iliyopigwa Uwanja wa Chamazi..Chanzo Global Publishers Blog

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)