SEMINA YA FURSA YAFANYIKA LEO MORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SEMINA YA FURSA YAFANYIKA LEO MORO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwansiti Almasi,akifafanua namna
anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia kundi lao
la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya
ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
Meneja huduma wa Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland
hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro
pamoja na Iringa.

wakifuatilia 
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.

 Semina ikiendelea ndani ya ukumbi . 
 Niki wa Pili akielezea fursa mbalimbali wanazoweza kuzitumia vijana katika
nafasi mbalimbali wanazozipata,badala ya kubweteka na kusubiri fursa
ziwafuate hapo walipo,na pia amewataka vijana wenzake waache kulalama
kila kukicha na kuona maisha ni magumu,badala yake wanapaswa kujituma
kwa kila nafasi waipatayo.
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa na wadau ukumbini humo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MaxMalipo,Bwana Ahmed Lussapi akizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye kampuni yake,na pia namna ya kunufaika nalo,amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo imekuwa ikiisaidia jamii katika wigo mpana kwa kutoa huduma mbalimbali,hivyo amewataka vijana  kuchangamkia fursa za namna hiyo ili kujikwamua na ugumu wa maisha.
 Mbunifu wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali
aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki
wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake
alizozidizaini kwa ubunifu wake.
 Mrisho Mpoto akisisitiza jambo.
 Mkali wa kughani Mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Morogoro  waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa twendzetu ndani  ya ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema  leo asubuhi
 Baadhi ya wageni waliohudhuria semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili akizungumza mbele ya  wakazi wa Morogoro wakati wa semina ya Fusra kwa vijana ikiendelea
ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo  asubuhi.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media  Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya
nane,ikiwemo  Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja  na Iringa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages