NA MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAA: MAN U WAIBUKA WABABE DHIDI YA BAYERN LEVERKUSEN KWA KUWATUNGUA MAGOLI 4 KWA 2 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NA MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAA: MAN U WAIBUKA WABABE DHIDI YA BAYERN LEVERKUSEN KWA KUWATUNGUA MAGOLI 4 KWA 2

Hatimaye Dakika 90 za Mchezo zimeweza kumtangaza na kuamua bingwa wa Mchezo wa leo Kati ya Manchester United dhidi ya Bayern Leverkusen. Mchezo uliochezwa kwa ustadi wa hali ya juu kwa timu zote mbili na kupelekea Man U kuibuka Mshindi wa Mechi hiyo kwa Kuwatungua Bayern Leverkusen Magoli 4 Kwa 2

Manchester United ndio walikuwa wa kwanza kuona nyavu za leverkusen kupitia kwa mshambuliaji wake Wayne Rooney katika Dakika ya 22 ya Mchezo kipindi cha Kwanza na kupelekea goli hilo kudumu kwa takribani dakika 22 mbele, dakika 17 baada ya Wayne Rooney kuiandika Goli timu yake Mchezaji wa Man U Robin Van Persie alipewa kadi ya njano.

Dakika ya 54 kipindi cha Pili Bayern Leverkusen waliweza kupata goli la Kusawazisha kupitia kwa mchezaji wake Simon Rofles na kupelekea timu hizo kuwa sare ya goli 1 kwa 1.

Dakika 5 mbele Mchezaji wa Man U Robin Van Persie aliweza kuiandikia timu yake ya Man U goli la 2 dhidi ya leverkusen na Kupelekea Man U kuwa mbele kwa Goli dhidi ya Leverkusen

Dakika ya 70 Man u waliweza kupata goli la tatu kupitia kwa Mchezaji wake Wayne Rooney na kufanya Man U kuwa na Magoli 3 kwa 1 dhidi ya Levekusen

Dakika 9 Mbele Mchezaji wa Man U Antonio Valencia aliweza kuiandikia Man U goli la 4 na la ushindi dhidi ya Leverkusen

Dakika ya 88 leverkusen waliweza kupata goli la 2 na kupelekea matokeo kuwa Man U 4 Vs Leverkusen 2.

Hatimaye Man u waibuka na ushindi mnono kwa kuwatungua Leverkusen magoli 4 kwa 2 na mpira umekwisha


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages