KUMBUKUMBU YA MIAKA 6 YA KIFO CHA MZEE SHAURI TIMOTHEO NATHAN - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUMBUKUMBU YA MIAKA 6 YA KIFO CHA MZEE SHAURI TIMOTHEO NATHAN

Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007)
  
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika mitano sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/09/2007 saa kumi na mbili jioni.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki "Father Kidevu".

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.

Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Imanuel Kajiru, Eliewaha Kajiru, Timothy Kille, Maria Thomas, Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan
Dossa, Dinner Onesmo,Digna Onesmo, Debora Daniel na  Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani, Kidai na Shauri.

Wananchina majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro piawanakukumbuka sana pamoja na wote wa Ugweno, Kilimanjaro.
Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa "TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE," baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.


Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages