Picha Kwa Hisani ya Mwanahabari Uswazi Blog
Ajali
mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita
karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land
cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya
mjini musoma kuelekea kamnyonge.
Kamera
yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa
anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache
askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na
kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.
Mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la
tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia
abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali
iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
Mmoja
wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa pikipiki Wambura Matiku aliyekuwa
nyuma ya pikipiki iliyopata ajali aliiambia blog hii dereva wa pikipiki
mara baada ya kulipita gari hilo aliwahi kuingia upande wa gari na
kutokea kwa ajali hiyo.
Hata
hivyo jeshi la polisi mara baada ya kumuwahisha majeruhi huyo
hospitalini walirejea eneo la tukio na kupima ili kubaini chanjo cha
ajali hiyo huku Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui akiahidi
kuitolea taarifa mara baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.
UWIIIIIIIIIIIII...SO SAD.......JAMANIIIIIIIIIII'''
ReplyDelete