Na Mwandishi Wetu
WAKATI
zikiwa zimebaki siku tatu ili Redd’s Miss Tanzania ajulikane, viingilio kwa
ajili ya shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi vimetangazwa.
Kiingilio
cha juu katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa (Jumamosi) katika
Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ni Sh 100,000 kwa viti
maalumu, huku viti vya kawaida vikiwa Sh 50,000.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redd’s
Original, Victoria Kimaro, ambao ndio wadhamini wakuu wa Redd’s Miss Tanzania
alisema, wanaamini viingilio hivyo ni vya kawaida kutokana na ubora wa shindano
lenyewe.
Victoria
alisema, burudani katika shindano hilo inatarajiwa kutolewa na msanii mahiri
kutoka Uganda, Mike Ross atakayeshirikiana na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’
pamoja na kundi la Mama Afrika katika kukonga nyoyo za mashabiki
watakaojitokeza ukumbini hapo.
“Tunaamini
kabisa wasanii hawa watakonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya urembo hapa
nchini, hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki kujinunulia tiketi mapema ili
kuepuka usumbufu,” alisema Victoria.
Naye Lady
Jadee alisema, kwa kushirikiana na bendi yake ya Machozi wamejipanga vizuri
kuhakikisha wanatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wote watakaohudhuria.
“Nawaomba mashabiki
wangu na wale urembo kujitokeza kwa wingi ili kufurahia burudani nzuri toka
kwangu na bendi yangu ya Machozi, pia wasanii wenzangu waalikwa naamini
watafanya vizuri siku hiyo,” alisema.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ambao ni waratibu wa
Redd’s Miss Tanzania alisema, tiketi za shindano hilo tayari zimeshaanza kuuzwa
katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Alitaja
maeneo ambayo yameteuliwa kuuza tiketi za Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu ni
duka la Shear Illusion lililopo Mlimani City, City Sports Lounge na Steers zilizopo
Mtaa wa Samora, Faberk Fashion, Rose Garden Pub na ofisi za Redd’s Miss Tanzania
ambazo zote zipo eneo la Mikocheni.
“Kwa mara nyingine
tena napenda kuwashukuru wadhamini wetu wakuu
kinywaji cha Redd’s Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli
wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri na
lenye tija kubwa.”
Lundenga
alifafanua kuwa, ili kuwapa fursa watu wengi zaidi tiketi itakayonunuliwa
katika vituo vilivyopangwa kabla ya shindano itakuwa ni Sh 80,000 na kutakuwa
na ofa kadhaa.
Taji la
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyefanikiwa
kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Shindano la
Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original
kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku wadhamini
wenza wakiwa kinywaji cha Zanzi, hoteli ya Giragge, Star TV, gazeti la Nipashe,
Uchumi Supermarket na Marie Stopes.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)