Stori: Mwandishi Wetu
MWANAMKE raia wa Kenya, Naima Mohamed Nyakiniywa ambaye pia anatumia pasi ya kusafiria ya Tanzania ikiwa na jina la Mwanaidi Ramadhani Mfundo maarufu kama Mama Leila, ni adui mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama kutokana na madai kwamba amebobea kwenye biashara ya madawa ya kulevya.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Obama, ambaye pia baba yake mzazi alikuwa Mkenya, mwaka 2011
alimtaja Naima katika orodha ya watu saba yeye akiwa wa 6 kuwa ni
hatari kwa biashara hiyo haramu ya ‘unga’ ambapo pia aliamuru mali zake
na wenzake hao zilizoko Marekani kutaifishwa, pia wasiruhusiwe kukanyaga
ardhi ya taifa hilo kubwa duniani.
Septemba 16 na 17, mwaka huu,
Mama Leila (na wenzake nane) alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania
kwa mashitaka ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin, Juni
Mosi, 2011 Mbezi Beach jijini Dar.
Rekodi zinaonesha kuwa mwanamke
huyo alizaliwa Septemba 2, 1962, Majengo, Nairobi, Kenya. Ingawa ni
maarufu maeneo mengi ya mji huo mkuu wa nchi jirani, Pumwani, Majengo,
Kariokor, Kaloleni, Biafra na Bahati, lakini katika hali ya usiri
mkubwa, mwanamke huyo hafahamiki kwa majina ya Mama Leila, Naima au
Nyakiniywa, isipokuwa anafahamika kama Kanyanya.
Kanyanya anayedaiwa
kuwa mama wa watoto watano, katika eneo analoishi la Mbezi Beach jijini
Dar es Salaam anajulikana ni Mtanzania kutoka kabila la Wadigo na
majirani wanasema ni mtu mwema, mwenye moyo wa kusaidia walio na shida,
akiwa pia ni mfanyabiashara wa magari, saluni na ‘internet cafes’.
Nchini
Kenya, inadaiwa Kanyanya alikuwa mtu mwema katika eneo la Majengo huku
majirani wakisema hakukuwa na njaa katika eneo lolote ambalo Naima
alikuwepo na kila mtu alipata alichokihitaji.
Kutajwa kwake na Rais
Obama kunadaiwa kuwashtua wakazi wengi wa Nairobi ambako kama ilivyo
Mombasa na Dar es Salaam, anamiliki mali mbalimbali, yakiwemo majumba ya
kifahari.
Hata hivyo, mwaka 2009, Polisi wa Kenya walidaiwa
kuwakamata vijana watatu wakiwa na madawa ya kulevya na wote walimtaja
Naima kama ndiye mwenye mzigo lakini ilikuwa vigumu kwao kumuunganisha
kutokana na kukosa ushahidi.
Chanzo chetu kimethibitisha kwamba
wakati mmoja Naima aliwahi kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya na
kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani jijini Nairobi lakini
shinikizo kutoka ‘juu’ lilisababisha mwanamama huyo kuachiwa bila
kufunguliwa mashitaka.
Inadaiwa kuwa hata alipokamatwa Dar es Salaam
kwa tuhuma za kuhusika na biashara hiyo, kulikuwa na idadi ya simu za
kutosha kutoka ofisi ‘kubwa’ jijini Nairobi zilizotaka aachiwe lakini
polisi wa Bongo ‘walikomaa’ naye ili kumfahamu zaidi.
Naima anamiliki
zaidi ya hati sita za kusafiria zenye majina na sura tofauti ili
kufanikisha safari zake za mara kwa mara nje ya nchi na mojawapo ni ya
Tanzania ambayo haifahamiki ilipatikana kutoka ofisi gani ya uhamiaji
hapa nchini.
Katika orodha ya Rais Obama ya watu hao kutakiwa
kufilisiwa mali zao na kutokanyaga Marekani, pia yupo mbunge wa zamani
wa Jimbo la Kilome, John Harun Mwau kutoka chama cha siasa cha Party of
Independent Candidates of Kenya (PICK).
Wengine katika orodha hiyo ni
Manuel Torres Felix wa Mexico, Gonzalo Inzunza Inzunza (Mexico) Haji
Lal Jan Ishaqzai (Afghanistan), Kamchybek Asanbekovich Kolbayev
(Kyrgyzstan) na Javier Antonio Calle Serna wa Colombia.Chanzo: Global Publishers Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)