MH. BENDELA ASHAURI VYAMA VYA MICHEZO VIWE NA WADHAMINI WA KUDUMU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MH. BENDELA ASHAURI VYAMA VYA MICHEZO VIWE NA WADHAMINI WA KUDUMU

Timu mbali mbali zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwa kwenye Maandamano.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (Katikati) akiongoza maandamano hayo kuelekea kwenye Ukumbi wa Mashindano.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela amevitaka vyama vya michezo
nchini kutafuta mbinu ya kuwa na wadhamini wa kudumu kama ilivyo kwa
mchezo wa pooltable, badala ya kuka na kulalamikia kukosa wadhamini.

Rai hiyo aliitoa mjini hapa wakati akifungua michuano ya pool table
ngazi ya taifa inayofanyika kwenye ukumbi wa Tanzanite, nakwamba
mchezo huo umekuwa ukidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia
bia yake ya safari lager (TBL) katika kipindi cha miaka sita
mfululizo.

“ Baadhi ya vyama vya michezo vimekuwa vikilalamikia kukosa wadhamini
na kudai kuwa mchezo wa soka pekee ndo umekuwa ukidhaminiwa jambo
ambalo si kweli, nakwamba mbona chama cha chezo wa pool table taifa
kimeweza kuwa na udhamini katika kipindi kirefu. “ Alisema

Aidha Mkuu huyo wa mkoa alisema vilabu 17 kutoka mikoa 17 vinashiriki
michuano hiyo, ambapo kati ya wachezaji hao itaundwa timu ya Taifa
itakayo iwakilisha nchini mwakani kwenye mashindanohayo nchini Malawi

Aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu pamoja na kuupenda mchezo
wanaoucheza , nakwamba kwa kufanya hivyo kutawawezesha kujiongezea
kipato, kuiletea nchi sifa na kutolea mfano wa Bondia Francis Cheka.

Kwa Upande wake Meneja kutoka Kampuni ya Bia Tanzania Kupitia bia yake
ya Safari Lager Oscar Shelukindo, alisema kampuni hiyo itaendelea
kudhamini mashindano hayo, ambayo mwakani yatafanyika nchini malawi na kuwataka wachezaji kuondoa shaka.

Shelukindo aliwataka wachezaji kucheza kwa kujituma ili kupata
wachezaji wenye viwango vinavyotakiwa ili waweze kuiwakilisha nchi na
hatimaye kuibuka na ushindi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pooltable Taifa, Fredy Mushi
alisema mchezo huo unashirikisha vijana kuanzia miaka 18 na kuendelea,
ambapo umeendelea kukua na kuungwa mkono sehemu nyingi tofauti na
awali.

Alisema baadhi ya wachezaji wamekuwa wakisajiliwa na timu nyingine
kutoka mkoa hadi mkoa na hivyo kujiongezea kupato, hivyo kuwaomba
wazazi na wananchi kutoa ushirikiano, na kudai kuwa bila ushirikiano
wao ukuaji wake utashuka.

Hata hivyo alimpongeza mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Aziz Abood
kwa kununua meza kwaajili ya wachezaji mkoani hapa nakwamba ni jambo
la kuigwa na watu wengine wenye mapenzi mema na machezo huo.

Timu zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Morogoro, lindi,
Kagera, Tabora, Mwanza, Arusha , Shinyanga, Pwani, Temeke, Ilala,
Kinondoni, Mbeya Dodoma , Iringa , Mara, Mnyara na Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages