Kambi
hii ambayo imejumuisha warembo 15 kutoka mikoa nane ya Tanzania itakaa
kwa muda wa wiki moja katika hotel ya Urban Rose kabla ya kumpata
mshindi siku ya fainali ambapo itakuwa tarehe 27 mwezi Septemba mwaka
huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Ukilinganisha
na miaka mingine mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidogo ambapo
ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania kulikuwa na
washindi wa pili na watatu. Mwaka huu mshindi mwingine atavikwa moja kwa
moja taji la Miss Earth Tanzania na Mshindi wa tatu bora ndio atakua
runner up. Warembo watakaochuana kuwania taji hilo ni kama ifuatavyo na
mikoa waliyotoka kwenye mabano. Aziza Victoria(Dar es Salaam) , Irene
Nsiima (Dar es Salaam), Betty Boniface(Dar es Salaam), Kundi Mlingwa(Dar
es Salaam), Mariam Ngwangwa(Dar es Salaam) , Consolata Mosha( Mwanza),
Agnes Thobias, Dinah David ( mbeya), Upendo Dickson (Dar es Salaam),
Naomi Kisaka(Dar es Salaam), Glady Msemo(Dar es Salaam) , Vestina
Mhagama(Dar es Salaam) , Angela Lutataza(Dar es Salaam) , Clara Noor(
Mwanza), Sasha Lukiko(Dar es Salaam).
Timu
ya Compass Communications ilizunguka takriban Mikoa 8 ya Tanzania
kufanya usahili kwa kila mkoa ili kupata wawakilishi wa mikoani katika
kinyang’anyiro hiki. Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Mtwara,
Manyara, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Jumla ya washiriki
15 wataingia kambini kuchuana kumpata Mwakilishi wa Tanzania katika
fainali za dunia zitakazofanyika nchini Moscow,Urusi.
Mashindano
ya Miss Universe kwa hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo
Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika
kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, 2009
yaliwakilishwa na Illuminata James ambapo mwaka 2010 mrembo Hellen
Dausen ndiye aliyepokea kijiti, 2011 Nelly Alexandra Kamwelu na
anayekabidhi taji mwaka 2012/2013 ni Winfrida Dominique.
Mashindano ya Miss Universe yamedhaminiwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA), Fastjet, Mohamed Enterprises (MetL) na Wadhamini
wenza(Parters) ni CocaCola, Missie Popular Blog, Healthy Beauty Clinic,
Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog, AZH Photography.com na
Adams Digicom
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)