Mapacha Watatu Band FC, Mashujaa Band FC hakuna mbabe - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Mapacha Watatu Band FC, Mashujaa Band FC hakuna mbabe


 Kikosi cha Mapacha Watatu Band FC
Kikosi cha Mashujaa Band FC
MECHI iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mapacha Watatu FC na Mashujaa Band FC  imeisha vizuri huku timu zote mbili zikifungana bao 1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi linalopatikana kataika mtandao wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa ushirikiano na undugu kwa wanamuziki.
Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa kwa  wote walioishuhudia. Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
Mfungaji alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis Dacota aliyeichambua ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji mwalikwa Mathew Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza mpira wavuni.
Wachezaji wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid Chokoraa, Kasongo, Dacota , Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama lango la Mashujaa kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
Lakini Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba, Abdul Tall, Jado FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika Mapacha Watatu.

Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumalizika, Mashujaa walisawazisha kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya, ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi hilo la Bongo Dansi, lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo Said Mdoe, Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages