Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis pamoja na viongozi wengine, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Masoud (kulia), alionesha uso wa bashasha baada ya kuwasili nchini akitokea India. (picha na Salmin Said, OMKR)
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amewasili
nchini akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa
kawaida wa afya yake.
Katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Maalim Seif alipokelewa na
viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis.
Aidha
mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa
Chama Cha Wananchi CUF, yaliambatana na shamra shamra mbali mbali za
burudani.
Maalim
Seif aliondoka nchini tarehe 24 mwezi uliopita kuelekea India kwa ajili
ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake, utaratibu ambao umekuwa
ukifanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)