Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga, ambapo leo katibu Mkuu huyo ameendelea na ziara yake ya siku nne mkoani humo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuimarisha uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani ya ya Uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum wakicheza na nyoka pamoja na wanakukundi cha utamaduni kutoka jimboni humo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja akimlipa ujira wa shilingi elfu 10.000 Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye baada ya kumsaidia katika ujenzi wa Birika la kunweshea mifugo katika kata ya Didia, hata hivyo Kinana aliwapa fedha pia wajenzi wa birika hilo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Soko la Kata ya Didia lililojengwa katika kijiji cha Didia, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI»





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)