JK azindua miradi ya maji na umeme Sengerema - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JK azindua miradi ya maji na umeme Sengerema

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Katika kijiji cha Katunguru/Nyamtelela wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Kulia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa umeme wa MCC unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Geita wakati wa  hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambaza umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa wilyani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
 Mwakilishi wa Serikali ya watu wa Marekani Bwana Karl Fickenscher akitoa hati ya kukabidhi mradi wa MCC I kwa waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati wa  hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambaza umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Katikati akishuhudia ni Afisa mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Account-(MCC)Tanzania Bwana Bernard Mchomvu.
 Mwakilishi wa Millenium Challenge Account nchini Tanzania Bwana Karl Fickenscher akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua mradi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambazia umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa,Wilayani Sengerema leo. Kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kulia ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages