JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya
Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463
-----
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za
mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza
kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina
utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za
mikononi.
Kwa
kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale
ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya. JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika
kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa
kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ. Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo
wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa
kwa namna yoyote.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari
na Uhusiano
Makao Makuu ya
Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)