Huyu ndiye Musa Senkando,Mume wa Marehemu Yusta anaesadikika kufanya mauaji hayo na anatafutwa na polisi.
======================
Na Mwandishi wetu.
Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia(leo) jana.
“Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.
Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.
“Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.
Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)