Na Kenneth Kinonko wa Globu ya Jamii, Nairobi
Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa.
Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa.
Kupitia ujumbe wao katika mtandao wa twitter, kundi hilo limesema shambulio hilo ni ujumbe kwa Serikali ya Kenya kuitaka iondoe majeshi yake yote kutoka Somalia. Kundi hilo pia limedai kuwa limeua watu zaidi ya idadi inayotajwa na vyombo vya usalama vya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema serikali bado haijabaini ni nani wamehusika na shambulio hilo.
Wakati huo huo idadi ya watu wanaosadikiwa kuuwawa imetajwa kuwa ni 30 na zaidi ya 50 wamejeruhiwa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa
Wateja wakihaha ndani ya duka hilo
Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba
Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha amedhakufa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)