Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Madai hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa Rwanda.
Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.
"Unajua ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja wa Uingereza, James Parker wa North London.
Mdadisi mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo ka Afrika Mashariki.
"Kutimuliwa kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam Hayes.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)