Mwanafunzi wa chuo cha St. Joseph, Goodluck
Msongore (23) akipokea zawadi ya Samsung LCD flat screen ya inchi 40 kutoka kwa
Afisa Mtandao wa Kijamii wa Tigo Bi. Samira Bamaar katika hafla fupi iliyofanyika
jana. Akishuhudia ni Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga. Tigo imetoa flat screen hizo kama zawadi kwa
washindi wa wateja wake wa Facebook waliojitokeza kushiriki mashindano ya
kampuni hiyo iliyokuwa inasherekea ukarasa wake wa Facebook kufikisha zaidi ya
watu 200,000 (laki 2) hivi karibuni.
Mshindi wa pili, Steven Kisaru (22) ambaye ni
mfanyakazi wa bandari Dar es Salaam akipokea kwa furaha remoti ya flat screen Samsung
LCD yenye inchi 40 na thamani ya shilingi milioni 2 aliyojishindia kutoka
katika ukurasa wa Facebook wa Tigo. Anayemkabidhi ni Afisa Mtandao wa Kijamii
kutoka Tigo Bi. Samira Bamaar, huku Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga
akishuhudia. Katika mashindano hayo wateja wengine walijishindia simu za
Samsung Galaxy S4, Ascend Y300 pamoja na modem na vocha kutoka Tigo.
Afisa Mtandao wa Kijamii kutoka Tigo Bi. Samira
Bamaar (kulia) akimkabidhi mshindi wa pili Marty Lyanga (25) flat screen aina
ya Samsung LCD mpya kabisa yenye thamani ya shilingi milioni 2. Marty ni mwanafunzi
wa Information Management katika chuo cha Tumaini, Dar es Salaam. Akishuhudia ni
Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga.
Mwanafunzi wa Bandari College, Daffd Laurent (20),
akionyeshea flat screen yake mpya aina ya Samsung LCD ya inchi 40 aliyejishindia
katika ukurasa wa Facebook wa Tigo. Kulia ni Afisa Mtandao wa Kijamii kutoka
Tigo Bi. Samira Bamaar. Tembelea ukurasa wa Tigo Facebook uweze kupata habari
na kujishindia zawadi mbali mbali pitia www.facebook.com/TigoTanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)