Na Waandishi Wetu
HAKUNA ubishi kwamba Taifa la Tanzania lipo kwenye mtikisiko mkubwa kufuatia kushamiri kwa matajiri wanaouza madawa ya kulevya ‘unga’ na watumiaji wake, Risasi Jumamosi lina mchongo mzima....Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapo palipoandikwa BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Hali ni mbaya kila kukicha, Watanzania wanakamatwa sehemu mbalimbali za dunia wakiwa na madawa hayo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi za Kitanzania.
Watumiaji nao wanaongezeka, mfano ukiwa ni mastaa kama Rehema Chalamila ‘Ray C’, Msafiri Diouf na wengine kibao ambapo pia vifo vinavyotokana na matumizi ya unga vinazidi panda chati.
MAKUNDI YA WAUZA UNGA
Mpaka sasa, watu wanaotajwa kufanya biashara ya kuuza madawa ya kulevya ni wale wenye majina makubwa wakidaiwa kuwatuma vijana wadogo, wa kike na wa kiume, hasa wenye majina au mastaa.
Matajiri hao, wengi wana majumba ya kifahari jijini Dar es Salaam, miradi mikubwa ya biashara na magari ya kifahari huku wakiishi maisha kama wapo peponi.
WANAFUNZI WALIVYOSALIMISHA MZIGO WA UNGA KWA MCHUNGAJI
Katikati ya wiki hii, wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na St. Gasper cha Morogoro walisalimisha kilo tano za unga aina ya Heroine na kuwataja vigogo kadhaa wa Tanzania kwamba ndiyo mabosi.
Wanafunzi hao walifikia uamuzi huo kwenye kongamano la Injili lililofanyika kwenye Ukumbi wa TAG, mkoani Mbeya chini ya Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste jijini humo. MAWAZIRI, WABUNGE SIRI NJE BIASHARA YA UNGA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi hao bila kumung’unya maneno wala kutoa sauti ya chini walitawaja kwa majina mawaziri wawili, naibu waziri mmoja, wabunge watatu wa viti maalum, wabunge wastaafu na baadhi ya wachungaji.
KONGAMANO LATAHARUKI
Hali hiyo ilisababisha watu waliokuwepo kwenye kongamano hilo wataharuki wakiwa hawaamini walichokisikia, hasa majina ya vigogo hao.
WALIOTAJWA MATATANI
Juzi, gazeti hili lilimtafuta Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili azungumzie sakata la vigogo hao kutajwa majina, lakini bila mafanikio.
Akizungumza na gazeti hili kwa masharti ya jina lake kutotoka gazetini, afande mmoja wa kikosi hicho ambaye si msemaji alisema Jeshi la Polisi limeyanasa majina ya vigogo hao na muda wowote watawaita kwa mahojiano.
“Majina yaliyotajwa na wale wanafunzi tunayo, tutawaita wahusika na kuwahoji,” alisema afande huyo.
WATOTO WA VIGOGO WATAJWA
Sakata la madawa ya kulevya pia limekuwa likidaiwa kuratibiwa na watoto wa baadhi ya vigogo wa ngazi za juu nchini huku ikielezwa kuwa ndiyo maana vita yake imekuwa ngumu.
Wengi waliozungumza na gazeti hili walitolea mfano kunaswa kwa watoto wawili wa aliyewahi kuwa kigogo wa BOT, Amatus Liyumba, Monalisa Liyumba ambaye alinaswa Juni 27, mwaka jana na Polisi wa Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Kitengo cha Kuzuia Madawa ya Kulevya akitokea Qatar.
Aidha, mapema mwaka jana mtoto mwingine wa Liyumba, Moreen alikamatwa nje kidogo ya Mkoa wa Lindi akihusishwa na madawa ya kulevya. Familia yake imekuwa ikimtembelea mara kwa mara mahabusu anakoshikiliwa.
WACHINA WAANZISHA X- RAY YAO MAALUM KWA WABONGO TU
Habari zilizosambaa mitandaoni hadi tunakwenda mitamboni ni Nchi ya China kuanzisha X-ray maalum kwa ajili ya Watanzania wanaoingia nchini humo.
Inadaiwa kutokana na mbinu za hali ya juu wanazotumia Wabongo wanaobeba unga na kuingia nchini humo, kipimo hicho ndiyo ‘komesha yake.’ MADEE ASIMULIA ALIVYOVULIWA NGUO UWANJA WA NDEGE WA SAUZI
Jumatano iliyopita, mwanamuziki wa Bongo Fleva na memba wa Kundi la Tip Top Connection, Hamad Ali ‘Madee’ alijikuta akiadhiriwa katika Uwanja wa Ndege wa Johannesburg, Afrika Kusini baada ya kukaguliwa hadi kuvuliwa t-shirt akidhaniwa amebeba unga.
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Madee alisema tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki hii ambapo baada ya kutua katika uwanja huo kila abiria alikaguliwa, lakini ilipofika zamu yake na kujulikana kuwa ni Mtanzania walimweka pembeni na kuanza kumkagua kuanzia begi lake.
Wahusika hao waliendelea kumkagua mwilini na kumtaka avue t-shirt na kubaki na singlendi huku abiria wengine alioshuka nao wakipita kwa kukaguliwa kawaida.
Alisema baada ya kukaguliwa sana na kuulizwa maswali kibao kwa muda wa saa moja, ndipo walimruhusu kuondoka huku wakimuomba samahani kwa tukio hilo. MARAFIKI WA MASOGANGE KUBANWA
Wakati habari zinadai kuwa, Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ amewataja mabosi waliomtuma unga Sauzi hadi akakamatwa, taarifa za kipolisi zinasema kwamba marafiki wa karibu wa staa huyo anayesota rumande na nduguye, Melisa Edward nao watabanwa ili kujua uhusiano huo.
Marafiki wa Masogange wako wengi, akiwemo mjasiriamali Romi na Evance Komu aliyewahi kudaiwa ni mpenzi wa mrembo huyo.
MAARUFU WALIONASWA NA MADAWA YA KULEVYA MPAKA SASA
Mpaka sasa, watu wenye majina yanayojulikana Bongo ambao wameshanaswa na madawa ya kulevya ni Agnes Masogange (kesi yake mbichi, Sauzi), Sandra Khan ‘Binti Kiziwi (kahukumiwa miaka 5 jela, Hong Kong) na Saada Kilongo (kesi mbichi Kusutu, Dar).
Habari imeandikwa na: Sifael Paul, Gladness Mallya.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)