STENDI YA DALADALA MKOANI DODOMA YAANZA KUTUMIKA KAZI LEO WINGI WA DALADALA STENDI YAONEKANA NDOGO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

STENDI YA DALADALA MKOANI DODOMA YAANZA KUTUMIKA KAZI LEO WINGI WA DALADALA STENDI YAONEKANA NDOGO

 Abiria wakiwa tayali wameshuka katika Daladala baada ya kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma na kushushiwa Barabarani baada ya kukuta msongamano mkubwa katika stand mpya iliyoanza kutumika leo ya jamatini.
 Mmoja wa viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo Danny Msitewa akifafanua jambo alipokuwa akisoma majina na kuwapa namba za utamburisho wa nafasi za kuweka vibanda vyao katika stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma
 Wafanya biashara waliokuwa stend iliyokuwa ya muda ya daladala oil com wakikusanya bidhaa zao zilizosambazwa na tingatinga lililofika kubomoa vibanda walivyokuwa wakaifaanyia biashara zao ili kuwashinikiza kuondoka eneo hilo.
 Asikari akitoa maelekezo kwa baadhi ya watu waliokuwa wakivizia kukwapua mali za watu zilizozagaa stand ya Daladala ya oil com Baada ya kubomolewa vibanda vyao ili wahame katika eneo hilo.

 Mwenyekiti wa Mipango miji na Mazingira manispaa ya Dodoma Stephen Mwanga akiwatangazia wafanya biashara ndogondpgo kutoendelea na ujenzi mpaka baazi ya taratibu zitakapokamilishwa.
 Msukuma Tololi akiingiza moja ya vibanda vya wafanyabiashara katika Stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma iliyoanza kutumika leo 

 Magali ya Daladala yakisubili abiria  ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
 Daladala zikisubili kuingia ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo. 
 Kazi ya bomoa bomoa ikiendelea stend ya mkoa

Na John Banda, Dodoma
MWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji
wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.

Mwenyekiti huyo aliwataka kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.

Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo haujaanza Augost 2012.

Alisema alipofika na kujionea kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.

'' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga

kwa upande wao baadhi ya Machinga hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.

TATIZO LA UDOGO WA STEND LAIBUKA

WAKAZI wa manispaa ya Dodoma wamelalamikia udogo wa Stand kuu ya Daladala ya Jamatini na kuitaka mamlaka nayohusika kuliacha eneo la oil com zilikokuwa zikipakilia abiria wakati wa ujenzi wa stand hiyo kuwa mbadala kutokana na wingi
wa magari.

Kauli hiyo ilitolewa wakati stendi hiyo ilipoanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza jana ambapo ilishuhudiwa wingi wa magali hayo ya Abaria yakiingia na kutoka huku kukiwa na msongamano mkuwa kiasi cha mengine kushushia abiria Barabarani.

Mmoja wa Abiria wanaotumia stand hiyo Winnie Binamu alisema imejengwa vizuri lakini haikidhi haja kutokana na kuwa ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya Daladala zilizopo hali inayosababisha msongamano na wengi kushusha abiria bila utaratibu ilimradi wawahi kupakia wengine.

Winnie aliongeza kuwa niafadhali kama wahusika wangeiacha stand iliyokuwa ikitumika kwa muda ya oili com kuendelea kutumiwa na baadhi ya magali ya njia nyingine na mengine kupelekwa jamatini kwa sababu kwa sasa watu ni wengi tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa upande wao madereva wa Daladala hizi walisema stand pamoja na uzuri haikidha kutokana na njia moja kuwa na magali zaidi ya 50 wakitolea mfano njia ya Chang'ombe, Mipango, UDOM, na kisasa zenye abiria na Magali Mengi.

Mmoja wa madereva wa Daladala zinazoelekea Ipagala Moses Mamba alisema kwa sasa Dodoma inawatu Wengi walioletelezwa na vyuo pamaja na taasisi zilizo na zisizo za kiserekali zinazoendelea kuhamia mkoani hapa hivyo ni vyema swala la stand hiyo kuangaliwa upya na ikibidi iwekwe ya ziada.

'' Ona ndugu mwandishi leo ni siku ya kwanza stand hii kuanza kutumika lakini msongamano ni kama unavyoona wengi wanashushia abaria barabarani kuanzia hapa yanapoingilia maka karibu na kipita shoto[ Round About] cha stand ya mabasi ya mkoani je wakija wote kutokana na tunavyojua itakuwaje?'', Alihoji Mamba

Katibu wa Umoja wa wenye Daladala [UWEDO] Peter Kabome alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi ni kama inafanyiwa majaribio kwa sababu haiwezekanai yakatakiwa kuingizwa magali zaidi ya 300 kwenye eneo linalochukua magali yasiyozidi 100.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango iji na Mazingira manispaa Stephen Mwanga alisema ameona msongamano huo jinsi ulivyo mkubwa hivyo atahakikisha anavihusisha vyombo vinavyohusika kikiwemo SAMATRA ili waweze kuona nini cha kufanya ili walau kuliweka sawa la staend hiyo.

PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA JOHN BANDA, DODOMA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages