Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wekundu
wa Msimbazi , Simba wameendelea na harakati zao za kutafuta beki mzuri
wa kati, na leo hii wamemsajili beki wa kimataifa raia wa Uganda, Joseph
Owino Gella kwa mkataba wa miaka miwili.
Owino
amesaini kwa mara nyingine Simba kwani aliwahi kuitumika klabu hiyo
kabla ya kuachwa na kujiunga na klabu ya Azam fc ambapo alishindwa
kulishawishi benchi la ufundi la wana lambalamba na akaamua kurejea
kwao Uganda na kujiunga na miamba ya soka nchin humoi, wakusanyaji wa
mapato wa URA.
Beki
huyo mwenye uwezo mkubwa wa kusimama katika safu ya ulinzi, amesaini
mkataba huo mbele ya makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, Joseph
Itang`are maarufu kwa jina la “Mzee Kinesi” na mjumbe wa kamati ya
utendaji Said Pamba.
Owino
aliyekuwa anaichezea klabu ya URA aliwavutia viongozi wa Simba wakati
wa mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya URA katika uwanja wa Taifa
ambapo Mnyama alilala 2-1, hivyo benchi la ufundi likaagiza nyota huyo
asajiliwe na ndipo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Kapteini
Zacharia Hans Poppe akamfuata na kuongea naye.
Mbali
na mchezo huo, Owino alionesha kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya
Yanga ambao walitoka sare ya 2-2 huku wanajangwani wakisawazisha dakika
za lala salama. Pia katika mechi dhidi ya Coastal Union uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga ambapo URA walilala 1-0, nyota huyo mwenye umbo
la mpira alionesha ufundi mkubwa na kuendelea kuwachanganya viongozi wa
Simba.
Akiwa
jijini Dar es salaam wakati klabu ya URA ilikuwa katika ziara ya
kucheza mechi tatu nchini, Owino alikaririwa akisema yupo tayari kurejea
Simba kwani ni kama nyumbani, hivyo aliwakaribisha katika mazungumzo na
ndipo Hans Poppe akaonesha umahiri wake katika usajili leo hii amemwaga
wino Msimbazi.
Kutokana
na usajili huo, beki mwingine raia wa Uganda, Samuel SSenkoom
ametolewa kafara na sasa Simba kidogo roho zao zinatulia baada ya
kulamba dume la uhakika.
Tangu
mabeki Kelvin Yondan kuihama Simba na kujiunga na Yanga, wakati Juma
Nyosso hakuwa katika uhusiano mzuri na viongozi, safu ya ulinzi imekuwa
uchochoro sana na msimu uliopita safu hiyo ilishindwa kuhimili
mikikimikiki ya ligi kuu na ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo
walitolewa hatua ya mwanzo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)