NBC yazindua huduma za kibenki kwa kutumia fedha ya Kichina (Yuan) na Huduma ya Mawasiliano ya papo kwa papo ya wateja (Hotline Service) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NBC yazindua huduma za kibenki kwa kutumia fedha ya Kichina (Yuan) na Huduma ya Mawasiliano ya papo kwa papo ya wateja (Hotline Service)


 Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma mpya ya kifedha kwa kutumia fedha ya China (Yuan) ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Mizinga Melu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

 Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha NBC, William Kallaghe (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wenzake katika hafla ya uzinduzi wa huduma za kifedha za NBC kwa kutumia fedha ya kichina. Mgeni rasmi
alikuwa Balozi wa China nchini, Dk. Yu Youqing.
 Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. 
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya NBC, Jane Dogani akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Hotline Service inayomwezesha mteja wa NBC kuuliza maswali yake moja kwa moja kwa ofisa wa benki hiyo awapo ndani ya tawi la benki.
 Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo pia kwa sasa inaweza kupatikana katikan matawi ya NBC

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages