Muonekano
wa nje wa Hoteli ya LISBON wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza
lilipotokea tukio la wizi wa mali za mteja.(Picha na Zainul Mzige wa Mo
Blog).
Na.Mwandishi wetu.
Katika
hali isiyo ya kawaida Meneja Mawasiliano wa Pangani FM Bw. Abdallah
Mfuruki ameibiwa dola mia moja za Kimarekani, vitambulisho vya kazi na
lesse ya kuendeshea gari pamoja na shilingi laki moja na nusu za
Tanzania katika mazingira ya kutatanisha.
Tukio hilo limefanyika usiku wa manane akiwa amelala ndani ya Hoteli ya LIZIBON iliyoko wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Bw.
Mfuruki amesema kuwa aliibiwa vitu hivyo Agosti 15 mwaka huu ndani ya
hoteli hiyo aliyofikia mjini humo kuhudhuria mafunzo ya redio za jamii
kuhusu demokrasia na amani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na UNESCO pamoja na UNDP yanashirikisha maneja 25 wa redio za jamii nchini.
Amesema baada ya kuibiwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini Sengerema na kupewa RB Namba SEN /M/146.
Baada
ya kufika katika eneo la tukio na polisi kujionea hali halisi ya tukio
hilo, Mmoja wa Askari waliofika kushuhudia tukio hilo alikiri kuwa
hoteli hiyo imekumbwa na matukio hayo mara kwa mara akiwemo yeye kuibiwa
siku za karibuni akiwa amelala hotelini hapo. Amesema suala hilo linahitaji ushirikiano wa karibu ili kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kwa
upande wake Meneja wa Hoteli hiyo Bw. Sosipita Shadrak alipoulizwa na
mwandishi wa habari hizi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuonesha
kushangazwa na tukio hilo wakati akijua wazi chumba namba 207
alichompatia mteja wake dirisha lake lilikuwa bovu kwa muda mrefu.
Kitendo
hicho kimewasononesha mameneja wengine waliohudhuria mafunzo hayo na
kuiomba mamlaka husika kufanya jitihada za haraka ili sheria ichukue
mkondo wake na vitu hivyo vilivyoibiwa vipatikane kwa wakati muafaka. Wamesema
pia kuwa iwapo sheria haitatendeka iko haja kuandika au kutoa tamko
ambalo linaweza kuharibu jina la hoteli au wilaya ya Sengerema kwa
ujumla.Wanahabari
tunajiuliza ndio tuseme utawala wa hoteli ya LIZBON unashirikiana na
wezi au wenyewe ndio wanaoiba vifaa vya wateja? Kwa sababu kwa nini
wasichukue hatua ya kutengeneza dirisha hilo lililoharibika muda mrefu
la chumba namba 207 ambako kila wakati kunatokea matukio ya wizi?
Tunatumaini polisi watafanya kazi yao na mali za mwenzetu ziweze kupatikana na hatua zitachukuliwa kwa hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)