Meneja wa Idara ya Habari na Mawasilino TGNP, Lilian Liundi (wa pili kushoto) akifafanua jambo katika mkutano na wahariri
Baadhi ya wahariri kutoka vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP Baadhi ya wahariri kutoka vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP
Katika mkutano huo na wahariri TGNP imeainisha baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo mtandao huo umezipata, ikiwa mbioni kufanya tamasha la mwaka huu ambalo litafanyika Septemba 3 hadi 6 2013, Katika viwanja vya TGNP Mabibo.
TGNP inatarajia kutumia Tamasha la Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki mijadala ya wazi na kupaaza sauti zao, tamasha hili litashirikisha wanawake, wanaume, Vijana na watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya Tanzania na nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika.
TGNP imebainisha kuwa kupitia Tamasha hilo, wanawake na wanaume wanaoshiriki wanapata fursa ya kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi katika, uchambuzi wa sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na watendaji wa serikali kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji huduma ambazo zitamfikia kila mwananchi.
Pamoja na mijadala hiyo ya wazi, kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular tribunal) itakayoendeshwa na Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga sera, wanasheria, wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na wananchi walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria au kuathika na hukumu zilizotolewa. Aidha siku inayofuata kutakuwepo na Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na wanazuoni na wataalamu wa sheria na wananchi wote watapata fursa ya kushiriki kikamilifu.
Mijadala mingine italenga katika masual ya haki ya uchumi kwenye upatikanaji wa huduma za msingi za jamii kama maji, afya, elimu, miundombinu na haki ya jamii katika umiliki wa rasilimali ardhi. Aidha suala la Katiba mpya litapewa kipaumbele katyika mijadala itakayopfanyika ikiwepo kuendelea kudai ushiriki ulio sawia katika fursa na michakato iliyosalia kufikia kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)