Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohd akizungumza
na wawakilishi wa vyama vya siasa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar juu
ya suala zima la uboreshaji Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa Chama cha Wananchi CUF Salum Bimani akitoa mchango wake katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kufanikisha Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Viongozi wa vyama vya siasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Mohd alipokutana nao Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa Chama cha Wananchi CUF Salum Bimani akitoa mchango wake katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kufanikisha Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Viongozi wa vyama vya siasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Mohd alipokutana nao Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Khadija Khamis na Amina Shaibu wa Habari Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka viongozi wa vyama vya siasa
kushirikiana na kutoa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha
sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kauli
hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mohammed Abuod Muhammed alipokutana na wawakilishi wa vyama vya siasa
ofisini kwa ke Vuga.
Alisema
kuwa Serikali imeamua kuzifanya sherehe hizo kuwa za aina yake na
zinahitaji mchango wa kila mtu bila ya kuangalia itikadi ya vyama vya
siasa ili kuonyesha uelewa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini.
“Mapinduzi
yetu yanafikia nusu karne, tutafanya sherehe kubwa na tumeamua
kuyashirikisha makundi yote kuanzia hatua za awali wakiwemo viongozi
wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wafanya biasha, makampuni, taasisi
binafsi, waandishi wa habari na makundi mengine ili kufanikisha
sherehe hizo,” alisema Waziri Aboud
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa pili wa Rais alidokeza kuwa Mgeni Rasmi
katika Sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China na wageni
kutoka nchi za Afrika Mashariki, nchi wanachama wa SADC pamoja na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ulaya pia wamealikwa kushiriki.
Aidha
alisema katika shamrashara za sherehe hizo kutakuwa na ufunguzi wa
miradi mbali mbali ya maendeleo, uwekaji wa mawe ya msingi, makongamano
na utajengwa mnara maalumu wa miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Nae
katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Dkt Khalid
Salum Muhammed alisema kuwa katika kufanikisha sherehe hizo
kumeandaliwa vazi rasmi siku ya kilele cha sherehe hizo yenye rangi za
bendera ya Zanzibar.
Aliongeza
kuwa vipindi maalum na picha za mafanikio ya Mapinduzi katika kipindi
cha miaka 50 vitaendelea kuonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vya
Serikali na binafsi na changamoto zilizojitokeza ili kuweza kukabiliana
nazo katika kipindi chengine cha miaka 50 .
Mapinduzi
ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoongozwa na Marehemu Abeid Amani
Karume yatatimiza miaka 50 tarehe 12 Januari 2014 na kilele chake
kitakuwa katika uwanja wa Amaan
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)