MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA ATEMBELEWA NA BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA CHARLES STITH - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA ATEMBELEWA NA BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA CHARLES STITH


 Mhe.Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania,Tanzania House,Washington DC
Mhe.Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha pamoja na Mhe. Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchi Tanzania. Kulia ni Bw.Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC

Mhe.Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico ametembelewa na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Charles Stith Ubalozini Tanzania House Washington DC juzi Jumatano Agosti 27,2013. Balozi Stith alifika Ubalozi hapo kusalimiana na Balozi Mulamula na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kushika wadhifa wake mpya wa kuiwakilisha Tanzania nchini Marekani.

 Katika mazungumzo yao,Balozi Stith alionyesha dhamira kubwa na utayari wake kushirikiana na Mhe.Balozi Mulamula katika kujenga mashirikiano baina vyuo vikuu vya Marekani na vile vya Tanzania. Balozi Stith alimweleza Balozi Mulamula kwamba anaifahamu vizuri Tanzania na ni nchi ambayo amekuwa na mahusiano mazuri pamoja na watu wake akiwa Balozi na hadi sasa. Kwa msingi huo, Balozi Stith alibainisha umuhimu wa kuweka mkakati mahususi wa kukamilsha azma hiyo na kuahidi kwamba muda wowote kuanzia sasa yupo tayari katika kutekeleza dhamira hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages