IGP MWEMA AKABIDHI UENYEKITI WA SARPCCO NCHINI NAMIBIA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

IGP MWEMA AKABIDHI UENYEKITI WA SARPCCO NCHINI NAMIBIA.

1Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akimkabidhi kitara Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga kama ishara ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) baada ya Tanzania kumaliza uongozi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano maalumu wa wakuu hao uliofanyika nchini Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
2Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akiongozwa na Askari wa Namibia kuingia katika ukumbi wa mkutano ambapo alitumia fursa hiyo kukabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
3Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga baada ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO).(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
………………………………………………………………………..
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania IGP Said Mwema amekabidhi uenyekiti wa Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika SARPCCO baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja cha kuongoza umoja huo.IGP Mwema amekabidhi uongozi huo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nchi ya Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga wakati wa mkutano mkuu maalumu wa viongozi hao uliofanyika jana katika jiji la Windhoek na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka INTERPOL na SADC.
Akizungumza katika mkutano huo IGP Mwema alisema katika kipindi cha uenyekiti wake walifanikiwa kufanya Operesheni kubwa iliyojulikana kama Operesheni Usalama ambayo ilijumuisha umoja wa SARPCCO na ule wa Afrika Mashariki EAPCCO,operesheni ambayo ililitea manufaa makubwa katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
Alisema Nchi wanachama wanapaswa kuendeleza ushirikiano wao ili kuhakikisha kuwa ukanda wa kusini mwa Afrika unakuwa salama kwa kukabiliana na uhalifu hasa kwa kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha alisema katika kipindi hicho Tanzania iliweza kuandaa mikutano yote ya kamati tendaji za SARPCCO ambazo ziliweza kuibua maazimio mbalimbali ya kupambana na uhalifu ambayo yaliweza kupitishwa na kuwa mikakati endelevu katika kukabiliana na uhalifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga alisema atahakikisha umoja huo unakuwa imara na kupambana na uhalifu unaovuka mipaka kama vile wizi wa magari, wahamiaji haramu, usafirishaji wa fedha haramu na binadamu, wizi wa mitandao pamoja na madawa ya kulevya.
Naye Mgeni rasmi katika mkutano huo Waziri wa Usalama na ulinzi wa Namibia Immanuel Ngatjizeko alisema serikali ya Namibia itaendelea kushirikiana na umoja huo kwa kila hali ili kuhakikisha Nchi wanachama na Afrika kwa ujumla zinakuwa salama.
IGP Mwema alikabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO mwezi Septemba mwaka 2012 mjini Zanzibar kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika kusini ambapo kutokana na uenyekiti huo mikutano yote ya umoja huo ilikuwa ikifanyikia nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages