FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA RASMI MWISHO WA MWEZI HUU MLIMANI CITY - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA RASMI MWISHO WA MWEZI HUU MLIMANI CITY


  Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"

Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited

Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages