Wananchi Sasa Kupata Taarifa za Huduma za RITA kwa ‘Sms’ , Tovuti na Mitandao ya Kijamii - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wananchi Sasa Kupata Taarifa za Huduma za RITA kwa ‘Sms’ , Tovuti na Mitandao ya Kijamii


Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua jambo katika wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
======  ==========

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.

Katika huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba 15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.

Pia wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala hao, www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo itapunguza msongamano wa wananchi kujua taarifa mbali mbali za vizazi na vifo na nyinginezo zinaztotolwa na wakala hao.

Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo ni kwa nchi nzima na kuipongeza RITA kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Media Mobile kwa kutengeneza huduma hiyo yenye ubora wa hali ya juu.

“Huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu ili kupata taarifa hizo, sasa taarifa utazipata kiganjani, tena kwa kutumia simu yako ya mkononi, ni jambo la faraja na la kujivunia,” alisema Waziri Kairuki.

Alisema kuwa Wizara yao ina mpango wa kuanzisha utaratibu ambao utaongeza kasi ya usajili wa wananchi kwa wakala hao ambapo mwananchi hataweza kupata kazi mpaka awe na cheti cha kuzaliwa. Pia hata kwa watu wanaotaka kupata leseni za biashara, kujiunga na shule na shughuli nyingine mbali mbali watalazima kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Afisa Mtendaji Kuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa wameamua kujiunga digitali ili kwenda na wakati na mpango wao mkubwa ni kupanua wigo wa huduma zao kwa kaya zote.

“Tunataka kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza taarifa muhimu kwa wananchi, hii itaturahisishia hata sisi kujua ufanisi wa shughuli zetu na kukabiliana na changamoto mbali mbali,” alisema Saliboko.

Saliboko alisema kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yao na wananchi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages