Bondia
Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia
wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi
yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam
Bondia Thomas Mashal |
BONDIA Thomas Mashali amewafananisha mabondia wenzake, Mada Maugo na Kalama Nyilawila kama midoli kwa kuwakebehi kuwa hawana lolote.
Hatua
hiyo ya Mashali inatokana na awali kupondwa na Maugo kuwa hana uwezo na
ni heri akageukia biashara ya kuuza chapati, wakati Kalama akimkebehi
kuwa ni kibonde wake.Akizungumza
na mwandishi wa gazeti hili katika gym yake, Manzese, Dar es Salaam
jana, Mashali alisema mabondia hao hawana uwezo wa kupambana naye kwa
sasa na ni kama midoli kwake.
Mashali, ambaye atapanda
ulingoni Oktoba 30 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kuzichapa na Maugo,
yuko katika mazoezi makali kwa ajili ya pambano hilo kabla ya baadaye
kupigana na Nyilawila.
“Unajua hawa ni kama midoli
kwangu (huku akionesha midoli aliyoshika), na kwa kudhihirisha hilo
nitaanza na maugo Oktoba 30 kumuonesha kuwa hatakiwi kuzungumza
asichokijua,” alisema Mashali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)