SYLONA ANYAKUA TAJI LA MISS REDD'S TEMEKE 2013 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

SYLONA ANYAKUA TAJI LA MISS REDD'S TEMEKE 2013

1AMshindi wa Redds Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwa na mshindi wa pili,  Narietha  Boniface, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu,  Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe Dar es Salaam jana 1BMshindi wa Redds Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwa na mshindi wa pili,  Narietha  Boniface, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu,  Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe Dar es Salaam jana 3C
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangaza washiriki walioingia kwenye kumi bora ya Redds Miss Temeke jana.
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
MREMBO Sylona Nyameyo jana usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Temeke lililofanyika katika Ukumbi wa TCC Changombe, jijini Dar es Salaam.

Sylona aliye mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akisomea mambo ya sheria alifanikiwa kuwashinda warembo wengine na kufanikiwa kujitwalia taji hilo.

Katika shindano hilo lililokuwa na upinzani mkali, ulioambatana na burudani za kumwaga, ilishuhudiwa nafasi ya pili ikienda kwa Marietha Boniface, ambaye naye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUCHS).

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Latifa Mohammed ambaye amemaliza kidato cha sita mwaka huu, hivyo warembo hao kujihakikishia nafasi ya kuingia katika fainali za Redd’s Miss Tanzania.

Ushindani ulionekana dhahiri katika shindano hilo, ambapo warembo walikuwa wakichuana mno, huku mashabiki waliojitokeza hapo wakijikuta wakishangilia muda wote.

Akizungumza mara baada ya kuvikwa taji hilo, Sylona alisema amefurahishwa mno na matokeo hayo na atahakikisha hawaangushi wakazi wa Temeke katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.

“Nilijua toka mwanzo lazima niwashinde, maana nilijiamini na niliona nina vigezo vyote, sasa ni wakati wa kwenda kupambana katika Redd’s Miss Tanzania ili kurudisha heshima ya Temeke,” alisema.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages