|
|
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Supersport.com
Kocha wa mabingwa wa soka
nchini England, Manchester United, David Moyes ana mipango ya kujenga
falsafa yake binafsi Old Trafford, lakini akisisitiza kuwa ataendeleza
utamaduni wa klabu hiyo wa kushambulia zaidi ili kutetea ubingwa wao
waliotwaa msimu uliopita.
Kocha huyo wa zamani wa Everton amerithi matunguli ya mstaafu Alex Ferguson na anatarajiwa na mashabiki wengi wa United kuendeleza mafanikio ya kibabu ambaye ameiongoza klabu hiyo kutwaa mataji 20 ya ligi kuu, Makombe matatu ya Ulaya, makombe 11 ya FA, Makombe manne ya Ligi na Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
“Kocha yeyote ambaye angepewa nafasi hii anatambua kazi ambayo kocha wa zamani amefanya. Meneja aliyepita alikuwa wa aina yake, amepata mafanikio makubwa sana na ni changamoto kubwa sana”. Alisema Moyes ambaye hajawahi kutwaa taji.
“Kila nitakachofanya ndicho Moyes alifanya nyuma. Nitaendeleza utamaduni wa United, lakini natakiwa kuongeza falsafa yangu nikiwa kocha mpya”. Alisisitiza Moyes.Moyes aliongeza kuwa ana bahati ya kuichukua timu ikiwa ni mabingwa, hivyo ni nafasi kwake kuanza vizuri, hivyo atajitahidi kufanya vizuri zaidi.
“Nimekuja timu ambayo inatwaa mataji wakati wote. United ni timu ya makombe, nahitaji kuendeleza hili”. Alisema Moyes. Kocha huyo alisema ana uzoefu mkubwa sana na mambo hayo na anajua kuna makocha bora zaidi ambao wangemrithi Sir Ferguson, lakini anajiamini zaidi kwani Fergie alimuambia lazima umrithi na ajenge imani kuwa anaweza.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)