Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa
wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya
habari ofisini kwake.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya akiongea na waandishi wa habari.Picha na Habari na Mdau Joseph Mwaisango
--
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
hatimaye yatoa ufafanuzi na kupigilia Msumari maamuzi ya Kamati ya Ushauri
(RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.
Akitoa maamuzi ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa
Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu
wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake amesema Kamati
imeridhika na ushauri uliotolewa na Kamati ya Ushauri iliyofanyika Julai
4, Mwaka huu.
Kandoro amesema lengo la kukutana na kamati ya
ulinzi na usalama ni kutokana na kuibuka kwa maneno toka kwa baadhi ya Wananchi
ambao wanadai maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa
Mpya Mkwajuni Wilayani Chunya hayakuzingatia vigezo vya umbali wa baadhi ya maeneo.
Amesema katika kuliletea ufafanuzi jambo hilo
Mkuu huyo wa Mkoa alidai kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ushauri wakiwemo
Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti wao wameitwa ili kutoa maelezo kwenye
kamati ya Ulinzi kama endapo mapendekezo yaliyotolewa na RCC hayakuzingatia matakwa
ya wananchi.
Ameongeza kuwa baada ya Kamati ya ulinzi na
Usalama ya Mkoa kuridhika na maelezo ya wajumbe hao imebariki na kuamua kuwa
mapendekezo ya Kamati ya Ushauri yabaki vile vile kwa Mkoa mpya kuwa Songwe
inayotokana na Mto Songwe uliopita kila Wilaya zinazounda Mkoa huo ambazo ni
Momba, Mbozi, Chunya na Ileje.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)