Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United wamecheza mechi yao
ya tano katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya
Kitchee ndani ya uwanja wa Hong Kong na kuibuka na ushindi wa mabao
5-2.
Mechi
ya leo ilitakiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini Kocha wa
United, David Moyes alilazimika kuahirisha mechi kwa madai kuwa uwanja
wa Hong Kong ulikuwa mbovu kufuatia mvua kunyesha na uwanja kujaa
matope, huku ukiwa umetumika mfululizo katika michuano ya kombe
la Barclays la Asia.
Hali
ya uwanja siku ya jumamosi wakati wa fainali ya Sunderland na Manchester
City ilikuwa mbaya sana, lakini viongozi walijitahidi kufanya jitihada
za kurekebisha kabla ya mchezo wa leo. Kikosi cha Kitchee: Comi, Rodriguez, Rehman, Kei, Alkande, Belencoso, Wai, Annan, Yang, To.
Wachezaji wa akiba: Jianqiao, Wen, To, Fung, Quankun, Hau, Fai, Paramo, Lam, Deshuai, Lung
Waliofunga Magoli yao: Lam (53), Alkande (69)
Kikosi cha Manchester United: Amos, Evra (Buttner HT), Anderson, Smalling, Carrick (Jones 72), Young (Januzaj HT), Welbeck (Lingard HT), Fabio (Rafael 72), Cleverley, Zaha, Keane.
Wachezaji wa Akiba: Lindegaard, Rafael, Jones, Ferdinand, Giggs, Van Persie, Buttner, Lingard, Januzaj.
Waliofunga mabao: Welbeck (16), Smalling (22), Fabio (26), Januzaj (47), Lingard (80)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)