Wilfried Zaha akishangilia bao lake la dakika ya mwisho lililoinusuru Manchester United kuzama. Chini anafunga.
Danny Welbeck akipambana
Zaha akishangilia Osaka
Van Persie na Tatsuya Yamashita
Zaha akimuacha mtu chini
KOCHA David Moyes tayari amesema mwanzo
wa Ligi Kuu ya England utakuwa mgumu, Manchester United, ikipambana na
Chelsea na Liverpool ndani ya wiki mwishoni mwa mwezi ujao.
Wazi hakutarajia mechi za ziara dhidi ya
wapinzani Asia na Australia zitakuwa ngumu, ila habari ndiyo hiyo na
leo imenusurika kulala mbele ya Cereo Osaka baada ya kulazimisha sare ya
2-2.
Mechi za kujiandaa na msimu na kwa
kujiweka fiti kwa ajili ya msimu, lakini leo bao la Wilfried Zaha
limeinusuru United kupata kipigo cha tatu katika mechi nne katika ziara
yake ndefu.
Wenyeji
walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Sugimoto dakika ya 34, lakini
Shinji Kagawa akasawazisha dakika ya 54, kabla ya wenyei kupata bao la
pili dakika ya 63, lililofungwa na Minamino.
Shukrani kwake, Zaha aliyeifungia United bao la kusawazisha akiwa ndani ya sita dakika ya 91.
Kikosi cha Man United leo
kilikuwa: Lindegaard; Rafael/Fabio dk79, Smalling, Ferdinand,
Buttner/Evra dk79, Young/Cleverley dk79, Giggs/Lingard dk79,
Jones/Anderson dk46, Kagawa/Zaha dk58, Welbeck na Van Persie/Januzaj
dk69.
Cerezo Osaka: Jin Hyeon, Sakemoto, Fujimoto, Yama, Maruhashi, Yokoyama, Kusukami, Fabio, Sugimoto, Minamino na Edno.
SOURCE:MDIMUZI BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)